Kiongozi huyo amesema hii itakuwa fundisho kwa wanywaji wengine wa waragi kujua thamani ya uhai na hivyo kutia adabu na heshima.
Kiongozi huyo kwa jina Edwin Komakech ametoa amri hiyo alipokuwa akizungumza katika mkutano huko wilayani Amuru, yapata umbali wa kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Inasemekana baadhi ya watengenezaji wa 'waragi' wamekuwa wakichanganya sumu katika kinywaji hicho ambacho kwa Tanzania kinafahamika kwa jina la 'gongo' au 'piwa' ama 'ulanzi' na Kenya wamekipa jina 'chang'aa'.
Polisi nchini humo wameanza uchunguzi kubaini watu wanao-mix waragi brew na poison na kusababisha watu kudedi.