Maeneo yatakayokumbwa na gharama mpya:
- Magomeni ambapo ujazo wa lita 36 awali ulikuwa ni sh 23,544 sasa ni sh 29,535
- Kimara ujazo wa lita ulikuwa ni 36 kwa sh 23,544 bei mpya ni 29,535
- Tabata lita 20 kwa sh 13,080 sasa ni sh 15,935
- Temeke ujazo wa lita 43 kwa sh 28,122 sasa ni 35 kwa 28,685
- Ilala ujazo uliokuwa ni lita 36 kwa sh 23,544 sasa ni 35 kwa sh 28,685
- Katikati ya jiji ujazo ulikuwa lita 52 kwa sh 34,008 sasa ni 35 kwa sh 28,685
- Kinondoni 43 kwa sh 28,122 sasa ni 45 kwa sh 37,185.
- Kawe ujazo ulikuwa ni lita 52 kwa sh 34,008 sasa ni lita 41 kwa sh 33,785
- Boko lita 52 kwa sh 34,008 sasa ni 41 kwa sh 33,785
- Bagamoyo ilikuwa 31 kwa sh 20,274 na sasa ni 32 kwa sh 26, 135
Mipango:
Ifikapo Januari 31, 2010 au kabla ya hapo, DAWASCO inatakiwa kuongeza idadi ya wateja waliofungiwa dira za maji kutoka 39,000 hadi 104,000 ambapo wateja wote wa Kimara, Kibaha, katikati ya jiji na Boko wanapaswa kuwa wamefungiwa dira za maji. “Na hii ni kupitia kanuni za utendaji kama ilivyoelekezwa kwenye kifungu namba 13 cha mkataba wa ukodishaji kati ya DAWASCO na DAWASA," amesema Mary.
Habari kwa mujibu wa gazeti DarLeo.co.tz