wavuti.weebly.com
  • Front
  • News blog
  • Scholarship links
  • Job links
  • Blog roll

Letter from Barack Obama, U.S.A President : The beginning of the END of Operation Iraqi Freedom

31/8/2010

 
Picture
Barack Obama - President of The United States of America
Friend --

Tonight marks the end of the American combat mission in Iraq.

As a candidate for this office, I pledged to end this war responsibly. And, as President, that is what I am doing.

Since I became Commander-in-Chief, we've brought home nearly 100,000 U.S. troops. We've closed or turned over to Iraq hundreds of our bases.

As Operation Iraqi Freedom ends, our commitment to a sovereign, stable, and self-reliant Iraq continues. Under Operation New Dawn, a transitional force of U.S. troops will remain to advise and assist Iraqi forces, protect our civilians on the ground, and pursue targeted counterterrorism efforts.

By the end of next year, consistent with our agreement with the Iraqi government, these men and women, too, will come home.

Ending this war is not only in Iraq's interest -- it is in our own. Our nation has paid a huge price to put Iraq's future in the hands of its people. We have sent our men and women in uniform to make enormous sacrifices. We have spent vast resources abroad in the face of several years of recession at home.

We have met our responsibility through the courage and resolve of our women and men in uniform.

In seven years, they confronted a mission as challenging and as complex as any our military has ever been asked to face.

Nearly 1.5 million Americans put their lives on the line. Many returned for multiple tours of duty, far from their loved ones who bore a heroic burden of their own. And most painfully, more than 4,400 Americans have given their lives, fighting for people they never knew, for values that have defined our people for more than two centuries.

What their country asked of them was not small. And what they sacrificed was not easy.

For that, each and every American owes them our heartfelt thanks.

Our promise to them -- to each woman or man who has donned our colors -- is that our country will serve them as faithfully as they have served us. We have already made the largest increase in funding for veterans in decades. So long as I am President, I will do whatever it takes to fulfill that sacred trust.

Tonight, we mark a milestone in our nation's history. Even at a time of great uncertainty for so many Americans, this day and our brave troops remind us that our future is in our own hands and that our best days lie ahead.

Thank you,

President Barack Obama

Balozi wa Tanzania-Marekani, Maajar awasili kazini

31/8/2010

 
Picture
Balozi Mpya Nchini Marekani, bi Mwanaidi Sinare-Maajar akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania mjini Washington, DC mara tu alipowasili tarehe 31 Agosti 2010 (photo credit: Dj Luke blog/Vijimambo)

SISIEMU Trans, oyaaa, unakwenda?

31/8/2010

 
Picture

Tunajifunza kutokana na mgomo wa Afrika Kusini?

31/8/2010

 
Serikali ya Afrika Kusini imeongeza ahadi ya kiwango cha mshahara kwa zaidi ya milioni kwa wafanyakazi wa umma waliogoma.

Rais Jacob Zuma alitoa wito wa kuanza upya mazungumzo baada ya mgomo huo wa wiki mbili kusababisha shule na hospitali nyingi kusimamisha shughuli zake. Baada ya kuwa na mjadala mzito usiku kucha, wawakilishi wa serikali wameongeza malipo hayo kwa asilimia 7.5.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikitaka ongezeko la asilimia 8.6 na wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumanne usiku kuamua wakubali ongezeko hilo au la.

Zwelenzima Vavi, katibu mkuu wa shirikisho kuu la vyama vya wafanyakazi, Cosatu, aliiambia BBC kuwa walipambana vilivyo katika mazungumzo hayo ili kuishinikiza serikali iongeze mshahara kwa asilimia nane. Alisema ni uamuzi wa wanachama iwapo watakubaliana na ongezeko hilo.

"Jana usiku tulipambana vilivyo na mpaka kufika asubuhi haikuwezekana.. Nahisi itabidi mgomo kama huu wa takriban wiki moja au mbili ufanyike ndio Serikali itakubali matakwa yao."

"Swali ambalo wanachama wetu wanatakiwa kujibu kwa sasa ni: je ni muhimu-ukizingatia masuala yote hayo- au ni hatua ya ushindi katika kipindi tulichofikia sasa?"

Mgomo huu umeathiri zaidi mahospitali, ambapo wauguzi wa kijeshi na watu waliojitolea wakiendelea kuwahudumia wagonjwa.

Takriban wafanyakazi wa umma milioni moja waligoma.

Raisi Zuma amekuwa akikosolewa na wafanyakazi waliogoma kuwa alikuwa katika ziara ya kibiashara huko China, il hali wauguzi, walimu na wafanyakazi wengine wa umma apo mitaani wakitaka ongezeko la mishahara. Ilimbidi Raisi Zuma arejeshe mahusiano mazuri na vyama hivyo, ambavyo ni ngao muhimu, kabla ya kuwepo mkutano wa sera wa chama tawala, the African National Congress, katika kipindi cha wiki tatu.

credit: BBC Swahili

Najiuliza...
...ikiwa somo limeeleweka kwa Wafanyakazi wa Umma wa Tanzania na kwa Wananchi wasio Wafanyakazi wa umma lakini wanaotumia huduma za umma..

Ben Mkapa ataka Afrika iwe na msimamo imara wa ardhi

31/8/2010

 
Raisi Mstaafu wa Tanzania awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa amezitaka nchi za Afrika kutoyumbishwa na propaganda za mataifa ya Magharibi kwamba wimbi la Wachina kuwekeza Afrika linaweza kuwafanya Waafrika kupoteza ardhi yao.

Badala yake amezitaka nchi za Afrika kuweka mfumo mzuri wa majadiliano na Wachina, ili kushirikiana nao katika matumizi ya ardhi kwa lengo la kuzalisha kwa wingi na kukuza uchumi.
Picture
Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa African Forum Dk. John Tesha mara baada ya kumaliza mkutano wa Maraisi wastaafu na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana uliokuwa unaelezea mikakati ya maboresho ya ardhi barani Afrika. (photo: Mroki Mroki)
“Msije mkababaishwa kwamba wawekezaji Wachina wana lengo la kuwanyonya na kuwanyang’anya ardhi Waafrika.  Kinachotakiwa ni mpango mzuri wa kujadiliana nao na kuweka mfumo mzuri kwa manufaa ya kiuchumi,” alisema Mkapa baada ya marais wastaafu wa nchi za Afrika kumaliza mkutano wao Jijini Dar es Salaam jana.

Mkapa alikuwa akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusu propaganda zinazoenezwa na mataifa ya Magharibi ya kuzihadharisha nchi za Afrika kuwa Wachina wanaweza wakawanyonya na hata kuchukua ardhi yao.

"Jambo la muhimu nchi za Afrika zinapaswa kuchunguza na kujua ni mwekezaji gani ambaye ana uwezo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi haraka  na kuwaletea wananchi maendeleo, na siyo kuangalia ni nani watashirikiana naye" alisema Mkapa.
Akielezea mambo waliojadiliana kwenye mkutano huo, Rais Mstaafu wa Mauritus, Karl Offmann alisema suala la ardhi barani Afrika wameliona ni jambo nyeti ambalo linayumbishwa na misimamo mbalimbali ya kisiasa.

Offmann alisema hawawezi kusema kwamba suala la ardhi Afrika halijatumika vizuri katika kuwaletea maendeleo Waafrika ila wana wasiwasi kasi ya ongezeko la watu, inaweza kuleta matatizo zaidi katika miaka ijayo.

“Tunaposema idadi ya watu Afrika ni kubwa tunalinganisha na mabara mengine. Afrika imeonyesha kasi ya ongezeko la watu. Kwa mazingira hayo ni wazi matatizo yanaongezeka. Hali hiyo inaashiria kwamba sasa ni wakati wa kutatua matatizo yanayotokana na suala la umiliki wa ardhi,” alisema Offmann.

Offmann alisema tatizo kubwa kwa nchi za Afrika ni kuweka usimamizi mzuri wa ardhi ni mawasiliano duni kama vile barabara na reli, hivyo masuala hayo, yanayopaswa kuwekewa kipaumbele.

credit habari: Mwananchi

Jaji Mkuu aonya kuzungumzia kesi zilizo Mahakamani

31/8/2010

 
Picture
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Augustino Ramadhani. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amewaonya wanasiasa wanaozungumzia kesi mbalimbali zilizopo mahakamani, katika majukwaa ya siasa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Jaji Ramadhani  alitoa onyo juu ya kauli hizo  jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa semina ya siku tatu ya majaji  wa mahakama za nchi 12 za Afrika.

“Kesi zote zilizopo mahakamani hazitakiwi kuzungumziwa nje ya mahakama, mimi mwenyewe wakati kesi ya mgombea binafsi ilipokuwa mahakamani nilikuwa sitaki kuizungumzia nje ya mahakama,” alisema Jaji Ramadhani.  

Kuhusu hatua watakazochukuliwa watu wanaozungumzia kesi zinazoendelea mahamani, jaji Augustino alisema hawawezi kutoka mahakamani na kwenda  kuwashika watu na kuwafungulia kesi bali mtu anatakiwa kupeleka malalamiko juu ya vitendo hivyo ndipo watakapoyafanyia kazi.

Habari kamili ya semina ya siku tatu ya majaji wa mahakama wa nchi 12 za Afrika, isome katika Mwananchi

C.U.F: Kutumia helikopta kwenye kampeni ni kutokujali

31/8/2010

 
Picture
Mgombea mweza kwa kiti cha Uraisi Haji Juma Duni (katikati) pamoja na baadhi ya viongozi wa CUF wakiwa mkoani Kagera. Kushoto kabisa ni mgombea Ubunge jimbo la Bukoba Mjini, Christian Kasimbazi na mwisho kulia ni Katibu wa CUF manispaa ya Bukoba Swahib Magayane.
Mgombea mwenza wa Profesa Ibrahim Lipumba anayewania nafasi ya urais kupitia CUF, Haji Juma Duni ameponda utaratibu unaotumiwa na CHADEMA pamoja na CCM ambavyo vinawasafirisha wagombea wao wa nafasi ya urais kwenda kuomba kura kwa wananchi kwa kutumia usafiri wa Helikopta.

Aliviponda hivyo wakati wa mkutano wa Chama hicho wa uzinduzi rasmi kampeni za ubunge na udiwani mkoani Kagera ulifanyika kwenye viwanja vya uhuru vilivyoko ndani ya Manispaa ya Bukoba.

Akiwa ameongozana na mbunge wa viti maalumu wa chama hichu mkoani Kagera, Savelina Mwijage na wagombea wa nafasi mbalimbali za ubunge na udiwani akiwemo mwanasiasa machachari Feliciani, alisema mgombea anayeomba kura kwa wananchi kwa kupitia angani kamwe hawezi kuelewa matatizo na kero zinazowakabili wananchi walioko chini ya ardhi na namna ya kuzitatua.

Duni alisema hatua ya vyama hivyo ya kuwapitisha wagombea wao angani badala ya kuwapitisha chini ya ardhi inadhihirisha wazi jinsi gani vyama hivyo wasivyowajali wananchi wanaowaomba kura za kuwapa ridhaa za kuwaingiza ikulu.

Aliwaambia wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara kuwa kamwe CUF haitatumia utaratibu wa kuomba kura kwa kutumia helikopta, ijapokuwa CUF inao uwezo wa kuomba kura kwa kutumia helikopta.

Aliendelea kusema kuwa CUF itaendelea kufanya kampeni zake kwa kutumia magari kwa kuwa matumizi ya magari yanakiwezesha chama hicho kitambue kwa urahisi kero na matatizo yanayawakabili wananchi,” ndugu wananchi huwezi kupitia angani ukaelewa kero zinazowakumba wananchi” alisema Duni.

“Ndugu wananchi unapofanya kampeni kwa kupitia ardhini unapata uzoefu mkubwa sana, unaelewa kwa urahisi kero za barabara, unaweza kuelewa barabara zisizopitika na zinazopitika, wanaofanya kampeni kwa kupitia angani taarifa za kero zinazowakabili wananchi wanazisoma kwenye vitabu baada ya kuletewa”alisema mgombea huyo.

Duni aliwaomba wananchi wakipe chama hicho ridhaa ya kuingia ikulu ili kiweze kutekeleza ilani yake vizuri, alisema ilani ya chama hicho inaeleweka na inaonyesha mwelekeo mzuri wa kuinua hali duni ya maisha waliyonayo Watanzania.

Aliwaonya wananchi mkoani Kagera kuwa makini katika kuvichagua vyama vya kuongoza nchi, aliwaambia wasichague vyama ambavyo ni mali ya watu binafsi na ambavyo vinahubiri masuala ya udini na ukabila, alisema vyama hivyo ni hatari kwa maendeleo kwa kuwa vikiingia Ikulu vinaweza kufilisi nchi.

“Kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaofikiri vyama wanavyoviongoza ni mali yao, ukitaka kuelewa vyama hivyo angalia viongozi hao wanavyoteuana, ikitokea nafasi mtu wa kwanza kufikiriwa lazima mjomba kwanza au shangazi au ndugu yoyote wa karibu na viongozi na wengine wanafikiriwa baadae, ndugu zangu kuweni makini na vyama hivyo msichague wagombnea wao” alimaliza.

credit: Audax Mutiganzi, Bukoba via Michuzi post

Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi - Yusuf Makamba

31/8/2010

 
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amewachambua makada wa CHADEMA mmoja baada ya mwingine akiwemo Marando na Shibuda kwa akusema tuhuma zilizotolewa na CHADEMA ni matusi yasiyovumilika.

Alisema, makada wote walioitukana CCM katika mkutano huo wa
CHADEMA wapo katika kundi la watu wenye uelewa mdogo (Simple Mind People).
Picture
Yufus Makamba / Katibu Mkuu CCM
Kundi hilo ni miongoni mwa makundi matatu ya watu wenye uelewa na hivyo Makamba ana maana kwamba, viongozi wa Chadema wana akili ndogo.

Aidha CCM imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutosubiri barua ya malalamiko wakati chama kinapokiuka mwongozo wa maadili kwa vyama vya siasa, ichukue hatua kukiwajibisha chama kinachokiuka makubaliano hayo.

Makamba ambaye alikuwa akizungumza kwa ucheshi alisema amelazimika kulizungumza hilo kwa kuwa yeye binafsi hawezi kuvumilia kuona kiongozi wao akitukanwa.  “Hata kama ingekuwa ni wewe, unaona baba au mama yako anatukanwa, ungevumilia? Hakuna anayeweza kufanya hivyo na kama yupo dunia itamshangaa, kuna uvumilivu wa kisiasa unaokulazimu uvumilie chama kinapoguswa lakini si huu,” alisema Makamba.

Alitaja uvumilivu huo wa kisiasa kuwa ni kuvumilia pale chama pinzani kinapokukosoa katika masuala ya elimu, kilimo, huduma za jamii lakini si katika kejeli na matusi kwa kuwa yanakwenda kinyume na mwongozo wa maadili ya vyama vya siasa ambao kila chama kinapaswa kuufuata.

Makamba akisoma baadhi ya makatazo ya mwongozo huo alisema chama chochote hakitakiwi kufanya fujo, vurugu, kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji au vitisho katika kampeni na kuongeza kuwa kinyume cha makatazo hayo, ndicho walichokifanya makada hao.

Akimchambua kada John Shibuda, alisema, “eti (Shibuda) anasema CCM ni kama tairi bovu, sasa tujiulize, hivi tairi bovu ni nani kati yetu na yeye, Maswa (Jimbo alilokuwa akiliongoza kwa tiketi ya CCM) waligundua hili mapema, wakambwaga katika kura za maoni.  “Kwanza baada ya kuona maji marefu, alikacha kugombea urais na kumsifia Kikwete kuwa ana maadili, anafaa tena akachangia Sh 200,000, leo anasema CCM gari bovu, kaishiwa hoja,” alisema.

Kuhusu Marando alisema, “anapaswa amshukuru Kikwete, ninajua wenye kesi ya EPA si wakosaji bado ni watuhumiwa mpaka mwisho wa kesi, lakini hivi serikali ikamate watu hata kama ni tuhuma na wewe unawatetea, unatetea mafisadi?”

Katibu huyo wa CCM alihoji kwa kuwa Dk Willibrod Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi. Amesema, hajali hata yeye (Makamba) akiwekwa katika kundi la wenye akili ndogo baada ya waandishi kuhoji kwa nini naye anazungumzia majina ya watu.

source: TBC

Redio za Tanzania

31/8/2010

 
Cross posting this from Candy1World blog whom I fully agree with here, and share the lamentations.

Nimeamua kuongea kuhusu hili baada ya kuangalia CNN MultiChoice African Journalist Awards. I

t is absolutely amazing seeing people making great stories, going to the source of the story, getting the untold and etc. Also the person who took the overall award of this year 2010, Sam Rogers, she was getting the story about the albino killings in Tanzania though I didn't get a chance to see the documentaryOur neighbours Kenya did well in the awards ceremony; not only Kenya but also Mozambique, South Africa and all others.

When I switch on the radio and "tune", about 95% of all stations just do music. News will be read for about 5 minutes and it is done. Music is not the problem, the problem is Tanzanian radio stations [are] not interested in things happening around the world.

Kama mambo yenyewe ndio hivyo, awards zitakuja kweli huku? Au ndio awards za hukuhuku za kumwaga?... Au ndio wanaona hizi redio za nje, namaanisha BBC au Deutsche Welle or VOA, wakileta habari zao ndio inatosha?

I am just asking...

Ujenzi unaendelea....

31/8/2010

 
Picture
Zitto Kabwe katika Kijiji cha Bitale,Kata ya Bitale, Kigoma Kaskazini Tarehe 30-08-2010
Ni ujenzi wa mengi.
Ujenzi wa Demokrasia.
Ujenzi wa kuitambua haki ya mwananchi.
Ujenzi wa kujitambua tulikotoka, tuliko na tunakotakiwa kwenda.
Ujenzi wa kufahamu umuhimu wa kushiriki kampeni na kumchagua kiongozi akufaaye.
...na  ujenzi wa Nyumba ilee, ambao kwa sera nzuri, mjenzi anaweza kupata vitendea kazi bila ya ukiritimba.

Taifa la Tanzania bado lipo katika Ujenzi, naam, kila leo twahimizwa, 'kulijenga Taifa'.

picha zaidi za ziara ya kampeni ya Zitto Kabwe katika kijiji hiki zinapatikana katika blogu yake (bofya hapa)

Maziwa yaliyopigwa marufuku yanaendelea kuuzwa

31/8/2010

 
Enyi wanunuzi wa maziwa ya kopo au mnaowafahamu wenye watoto wadogo, watahadharisheni.

Habari toka DarLeo ilivyoripotiwa na Godfrey Ismaely:

Siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti Chakula na Dawa Nchini (TFDA) itoe tamko la kuwataka wafanyabiashara wa maziwa aina ya Nestle kusitisha uuzaji ili kuwanusuru watumiaji hasa watoto wadogo na madhara, zoezi hilo limeonekana kutotiliwa maanani na wafanyabiashara hao.

Maziwa hayo ambayo yanaingizwa hapa nchini kutoka katika nchi za nje yanasadikika kuwa hayana viwango vya kutosha kwa ajili ya matumizi ya watoto wadogo kutokana na kuwa na vimelea vinavyochangia watoto wenye umri mdogo kuota matiti.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa gazeti hili katika maeneo mbalimbali ya jiji yakiwemo Kariakoo na Buguruni umebaini kuwa, baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla na rejareja waliokataa kutaja majina yao wanaendelea kuyauza maziwa hayo.

Aina hizo za maziwa ambayo wafanyabiashara hao wanayauza bila wasiwasi ni pamoja na Nestle yenye nembo ya Lactogen 1 na Lactogen 2, yanayoonekana yametengenezwa katika nchi tofauti ambazo ni (Ufaransa, Afrika Kusini na Uholanzi).

Aidha mwandishi wa gazeti hili alipotaka kufahamu sababu za wafanyabiashara hao kukaidi agizo la TFDA miongoni mwao katika soko la Kariakoo aliyekataa kutaja jina lake alidai kuwa hawezi kuteketeza akiba yake ya maziwa ambayo alinunua kwa wingi bila kufahamu ni nani atamlipa gharama zake.

“Siwezi kufanya kazi ambayo kwangu haina manufaa mimi niliagiza mzigo wa kutosha halafu unasema niteketeze haya maziwa hivi kwanza hao TFDA walikuwa wapi? wakati maziwa ya Nestle yakiingia hapa nchini leo hii wanatuwekea pingamizi haiwezekani,” alidai mfanyabiashara huyo aliyekataa kutaja jina lake.

Hatua za kuyadhibiti maziwa yanayoingizwa hapa nchini kutoka nchi za nje yalianza kuwekewa pingamizi na TFDA baada ya taarifa mbalimbali kusambaa katika vyombo vya habari kuwa watoto watatu wenye umri kati ya miaka minne na miezi 15 walianza kuota matiti nchini China.

Kutokana na matumizi ya maziwa ya unga yanayotengenezwa na kampuni ya NASDAQ Synatra katika jimbo la Hubei kuwa na kiwango kikubwa cha vimelea zvinavyootesha matiti ya watoto kupita ya mtu mzima.

Hata hivyo baada ya mamlaka hiyo kuweka kizuizi katika biashara ya kuuza maziwa ya Nestle, hivi karibuni walinasa makopo 2,261 ya maziwa yanayodaiwa kuwa ni feki na kutoa tahadhari kwa wananchi kuepuka matumizi yake ili kuzinusuru afya zao.

Marehemu Mufti Mkuu, Sh. Harith bin Khelef azikwa

31/8/2010

 
“Innaa lillahi wainnaa ilayhi raajiuun”
Truly ! to Allah we belong and truly, to him we shall return”
Picture
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume (wa tano toka kushoto) akijumuika na Viongozi wengine katika swala ya Maiti ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Marehemu Sheikh Harith Bin Khelef, katika Msikiti wa Mwembeshauri leo.
credit photos: Othman Maulid Othman

Ajali ya Mabibo, dereva alikuwa anakwepa kukamatwa

30/8/2010

 
Ile ajali mbaya iliyotokea mwishoni mwa wiki katika maeneo ya Mabibo Mwisho jijini Dar es Salaam iliyolihusisha gari aina ya Hilux Sulf lenye usajili namba T365 BSH lililokuwa likiendeshwa na John Mhando (53) na kusababisha vifo vya watu 6 na wengine wawili wakiwa katika hali mbaya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ilitokana na dereva wa gari hilo kuwa katika mwendo kasi akijitahidi kukwepa kukamatwa baada ya kuwa alishasababisha ajali nyingine katika eneo la Manzese.

Mhando aligonga mtu ambaye hajajulikana hadi sasa na baada ya hapo alimua kupita ‘njia za panya’ ili kukwepa kukamatwa na askari wa usalama barabarani, akaamua kupita njia ya Mabibo, lakini hakufika mbali kwani alipofika Mabibo Stand alishindwa kulimudu gari kwa kutokujua njia ilikuwa imefika kikomo na asiweze kung'amua haraka mwelekeo wa kulipeleka gari lake ambalo tayari lilikuwa katika mwendo kasi.

Inasemekana kuwa hii ni mara ya nne kwa nyumba hiyo kugongwa na magari tofauti, hali inayowafanya wananchi washauri kuwekewa alama kuonesha kuwa eneo hilo ni mwisho wa barabara "dead end".

GMail is rolling out Priority Inbox!

30/8/2010

 
The ever growing, best eMail client the I have ever used is rolling out yet another service, this time a Priority Inbox. How does this one work? Read part of a post from GMail's official blog by Doug Aberdeen:

People tell us all that time that they’re getting more and more mail and often feel overwhelmed by it all. It’s time-consuming to figure out what needs to be read and what needs a reply. Today, we’re happy to introduce Priority Inbox (in beta)—an experimental new way of taking on information overload in Gmail.

People get a lot of mail that isn't outright junk but isn't very important, so we've evolved Gmail's filter to address this problem and extended it to not only classify outright spam, but also to help users separate this unimportant stuff from the important ones. In a way, Priority Inbox is like your personal assistant, helping you focus on the messages that matter without requiring you to set up complex rules.
Picture
Priority Inbox splits your inbox into three sections: “Important and unread,” “Starred” and “Everything else”:

As messages come in, Gmail automatically flags some of them as important. Gmail uses a variety of signals to predict which messages are important, including the people you email most (if you email Bob a lot, a message from Bob is probably important) and which messages you open and reply to (these are likely more important than the ones you skip over). And as you use Gmail, it will get better at categorizing messages for you. You can help it get better by clicking the or buttons at the top of the inbox to correctly mark a conversation as important or not important. (You can even set up filters to always mark certain things important or unimportant, or rearrange and customize the three inbox sections.)

Priority Inbox will be rolling out to all Gmail users, including those of you who use Google Apps, over the next week or so. Once you see the "New! Priority Inbox" link in the top right corner of your Gmail account (or the new Priority Inbox tab in Gmail Settings), click here to take a look (YouTube video).
Picture

Heavy Drinkers Outlive Nondrinkers - 20 yr old Study

30/8/2010

 
Kichaa kapewa rungu sokoni, mm mm mmh, wapo watu wataogea pombe. Viwanda vya bia vitachekeleaje?

Why Do Heavy Drinkers Outlive Nondrinkers?  Article by John Cloud / TIMES (copyright)
Picture
One of the most contentious issues in the vast literature about alcohol consumption has been the consistent finding that those who don't drink actually tend to die sooner than those who do. The standard Alcoholics Anonymous explanation for this finding is that many of those who show up as abstainers in such research are actually former hard-core drunks who had already incurred health problems associated with drinking.

But a new paper in the journal Alcoholism: Clinical and Experimental Research suggests that — for reasons that aren't entirely clear — abstaining from alcohol does actually tend to increase one's risk of dying even when you exclude former drinkers. The most shocking part? Abstainers' mortality rates are higher than those of heavy drinkers.

Moderate drinking, which is defined as one to three drinks per day, is associated with the lowest mortality rates in alcohol studies. Moderate alcohol use (especially when the beverage of choice is red wine) is thought to improve heart health, circulation and sociability, which can be important because people who are isolated don't have as many family members and friends who can notice and help treat health problems.

But why would abstaining from alcohol lead to a shorter life? It's true that those who abstain from alcohol tend to be from lower socioeconomic classes, since drinking can be expensive. And people of lower socioeconomic status have more life stressors — job and child-care worries that might not only keep them from the bottle but also cause stress-related illnesses over long periods. (They also don't get the stress-reducing benefits of a drink or two after work.)

But even after controlling for nearly all imaginable variables — socioeconomic status, level of physical activity, number of close friends, quality of social support and so on — the researchers (a six-member team led by psychologist Charles Holahan of the University of Texas at Austin) found that over a 20-year period, mortality rates were highest for those who had never been drinkers, second-highest for heavy drinkers and lowest for moderate drinkers.

Picture
The sample of those who were studied included individuals between ages 55 and 65 who had had any kind of outpatient care in the previous three years. The 1,824 participants were followed for 20 years. One drawback of the sample: a disproportionate number, 63%, were men. Just over 69% of the never-drinkers died during the 20 years, 60% of the heavy drinkers died and only 41% of moderate drinkers died.

These are remarkable statistics. Even though heavy drinking is associated with higher risk for cirrhosis and several types of cancer (particularly cancers in the mouth and esophagus), heavy drinkers are less likely to die than people who have never drunk. One important reason is that alcohol lubricates so many social interactions, and social interactions are vital for maintaining mental and physical health. As I pointed out last year, nondrinkers show greater signs of depression than those who allow themselves to join the party.

The authors of the new paper are careful to note that even if drinking is associated with longer life, it can be dangerous: it can impair your memory severely and it can lead to nonlethal falls and other mishaps (like, say, cheating on your spouse in a drunken haze) that can screw up your life. There's also the dependency issue: if you become addicted to alcohol, you may spend a long time trying to get off the bottle. 

That said, the new study provides the strongest evidence yet that moderate drinking is not only fun but good for you. So make mine a double.

Mashallah! Beautiful photo collections from around the world observing the Holy month of Ramadan

30/8/2010

 
Muslims across the world are currently observing Ramadan, a month long celebration of self-purification and restraint. During Ramadan, the Muslim community fast, abstaining from food, drink, smoking and sex between sunrise and sunset. Muslims break their fast after sunset with an evening meal called Iftar, where a date is the first thing eaten followed by a traditional meal. During this time, Muslims are also encouraged to read the entire Quran, to give freely to those in need, and strengthen their ties to God through prayer. The goal of the fast is to teach humility, patience and sacrifice, and to ask forgiveness, practice self-restraint, and pray for guidance in the future. This year, Ramadan will continue until Thursday, September 9th.

See below are some photos from Boston.com's Big Picture grande collection.
Picture
Thousands of Muslims gather in the Grand Mosque, in Islam's holiest city of Mecca and home to the Kaaba (center), as they take part in dawn (fajir) prayers on August 29, 2010, to start their day-long fast during the holy month or Ramadan. (AMER HILABI/AFP/Getty Images)
Picture
A Syrian Muslim girl stands at the top of Mount Qassioun, which overlooks Damascus city, during sunset and prays before eating her Iftar meal on August 22, 2010. (REUTERS/Khaled al-Hariri)
Please click here to visit the site to see the complete collection in which you can also submit your photos for the next publication! Peace to all Muslims! May Allah accept your genuine prayers!

Husband Day Care Center

30/8/2010

 
Picture
photo credit: PwaniRaha.com

Ipo haja ya kurekebisha Katiba ya Tanzania - Tendwa

30/8/2010

 
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, amesema kuna haja ya kuifanyia marekebisho katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili mawaziri wasitoke miongoni mwa wabunge.

Tendwa alisema hayo katika mahojiano maalum katika kipindi cha Jambo Tanzania kinarushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha Shirika la Utangazaji la aifa (TBC1).

"Unafahamu kwamba katiba hii tumeirithi kutoka kwa wakoloni na serikali imeshaifanyia marekebisho mbalimbali ambayo hata hivyo hayajagusa suuala la mawaziri kutotokana na wabunge. Wakati umefika wa kuifanyia marekebisho ili mawaziri wetu wasitoke miongoni mwa wabunge," alisema.

Ufafanuzi huo wa Tendwa ulikuja baada ya mwendesha kipindi kumwomba azungumziae swala la mgombea wa ubunge katika jimbo la Nyamagana, Laurent Masha ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, kumwekea pingamizi mgombea mwenzake kupitia tiketi ya CHADEMA.

Akijibu swali hilo Tendwa alisema "waziri lazima awe mbunge kutokana na mfumo wa katiba yetu na ndiyo maana tunapata baadhi ya mawaziri ambao hawana taaluma ya wizara wanazoziongoza.""Waziri anatakiwa awe na taaluma katika wizara husika, kama ni Waziri wa Afya anapaswa kuwa na taaluma ya afya na kama ni Waziri wa Miundombinu pia anapaswa kuwa na taaluma ya hiyo." alisisitiza.

Alifafanua kuwa kama kutakuwa na katiba itakayokuwa inaainisha mambo hayo, hata uwajibikaji wa Serikali utaongezeka kwa sababu Waziri atakuwa mtumishi wa Serikali, ambaye anaweza kuwajibishwa mara moja.

Alisema kitendo cha  Waziri kuwa Mbunge kinatoa nguvu zaidi kwake kumwekea mgombea mwingine pingamizi sababu ni rahisi kwake kufanya uchunguzi haraka kuhusu mpinzani wake kuliko mtu mwingine.

"Kuhusu suala la Waziri wa Masha, yeye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mgombea wa Ubunge lakini tumeona alivyomwekea pingamizi mgombea mwenzake, ingawa pingamizi ni haki ya raia wote akiwemo Waziri huyo, ila utata huu unaonekana wazi kwa sababu ya aina ya katiba tulionayo ambayo inamtaka Waziri awe mbunge kwanza," alisema.

credit: Jackson Odoyo na Salim Said/Mwananchi

Haiiiya! Slaa amwakia Kinana

30/8/2010

 
Mgombea kiti cha Uraisi wa Tanzania kupitia CHADEMA, Willibrod Slaa akiwa Mikumi, alimlipua mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM, Abdulahman Kinana, akisema kigogo huyo ana mkono katika biashara chafu za makampuni ya meli; akamtaka ajielekeze katika masuala ya kitaifa badala ya kumwandama yeye (Slaa). Akasisitiza kwamba ana ushahidi wa kauli zake, kwani hana historia ya kukurupuka.

Kauli hiyo ya Dk. Slaa inakuja siku moja baada ya Kinana kujibu mapigo ya makada wa CHADEMA, hasa Mabere Marando, ambao waliwataja hadharani vigogo wanaohusika na ufisadi mkubwa, huku CCM ikilalamika kwamba chama hicho cha upinzani kinatoa matusi.

Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CHADEMA, Marando alisema vigogo waliohusika na wizi wa EPA ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Rostam Azizi na Edward Lowassa, akasema waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi ni dagaa wanaoonewa ili kuficha madhambi ya wahusika wenyewe.

Juzi Kinana alijitokeza na kumbeza Dk. Slaa, kwamba anatumia lugha ya matusi kwenye kampeni kinyume cha makubaliano waliyosaini. Slaa jana alisema mtu akiiba anaitwa mwizi; na kumwita hivyo si matusi.

Taarifa imenukuliwa toka blogu ya Ansbert Ngurumo - Utakapojua hujui ndipo utakapojua!

Kampeni za Ndesamburo/CHADEMA huko Moshi

30/8/2010

 
Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo jana alizindua kampeni zake huku chama hicho kikimlipua mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete kikidai anatumia vibaya fedha za umma kukarabati Ikulu. 
Picture
Philemon Ndesamburo/CHADEMA akihutubia wananchi Moshi
Chama hicho kimedai kuwa katika kipindi cha miaka minne ya mwanzo ya utawala wake, serikali yake imekarabati Ikulu kwa zaidi ya Sh23 bilioni ukilinganisha na Sh9 bilioni alizotumia Rais wa Serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Kauli hiyo, iliyoegemea zaidi kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ilitolewa juzi na katibu wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro, Basil Lema katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho.

Uzinduzi wa kampeni hizo ulitawaliwa na kila aina ya shamrashamra, ikiwemo helikopta ya Ndesamburo ambayo ikizunguka angani mjini wa Moshi tangu saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 huku ardhini yakifanyika maandamano makubwa.

Maandamano hayo, yaliyojumuisha waendesha pikipiki, msafara wa magari na mamia ya wananchi, ulianzia eneo la Majengo na kupita katika mitaa kadhaa hadi viwanja vya Manyema vilivyopo kata ya Bondeni.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi na wafuasi wa CHADEMA, Lema alisema katika mwaka wa kwanza tu kuingia Ikulu, Rais Kikwete alikarabati makazi hayo ya rais kwa Sh6.1 bilioni ambazo ni fedha za walipa kodi.

“Lakini mkumbuke kuwa katika kipindi cha mwisho cha miaka mitano, mtangulizi wake (Mkapa) alikarabati Ikulu kwa Shilingi bilioni 9, lakini Rais Kikwete alipoingia tu Ikulu akaamua kukarabati Ikulu hiyo hiyo kwa Sh ilingi bilioni 6.1,” alidai Lema.

Lema aliainisha matumizi hayo ya ukarabati wa Ikulu kuwa ni Sh6.1 bilioni (mwaka 2006), Sh5.59 bilioni (mwaka 2007), Shilingi bilioni 5.71 (mwaka 2008) na shilingi bilioni 6.1 anazodai zilitumika kukarabati jengo hilo mwaka 2009.

Picture
Katibu huyo alisema kulikuwa hakuna ulazima wa kutumia kiasi hicho kikubwa cha fedha za umma, hasa ikizingatia kuwa ndio kwanza majengo hayo yalikuwa yametoka kukarabatiwa kwa Shilingi bilioni 9.

Halikadhalika katibu huyo alidai kuwa mwaka 2007 pekee, serikali ilitumia Shilingi bilioni 447 kununua magari ya Serikali, fedha ambazo zingetosha kuwalipa walimu mshahara wa kima cha chini wa Shilingi 500, 000.

Lema alifafanua kuwa fedha zilizotumika kukarabati Ikulu kwa miaka minne ya Rais Kikwete zingeweza kujenga zananati 600 za kisasa kwa thamani ya shilingi milioni 40 kwa kila Zahanati inayojumuisha pia nyumba ya mganga.

“Ukubwa huu wa matumizi ya serikali ndio unawafanya Watanzania waendelee kuwa masikini na njia pekee ya kuondokana na matumizi ya aina hii ni kuiingiza CHADEMA kwenye mamlaka ya kuongoza dola mwaka huu,” alidai.

Ndesamburo, ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2000, alisema endapo atachaguliwa tena kwa kipindi cha tatu ataweka kipaumbele katika sekta za afya, miundombinu ya barabara za lami, elimu na usalama mjini.

Ndesasumbo alisema endapo wananchi wataipa CHADEMA ridhaa ya kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, atahakikisha hakuna mwanafunzi anayefaulu kwenda sekondari ambaye anashindwa kufanya hivyo kwa kukosa ada.

credit: Daniel Mjema, Moshi/Mwananchi

Waziri Ngeleja azuru Geita walimoripotiwa kufa wa 4

30/8/2010

 
Imeripotiwa kuwa watu wanne walifariki na wengine sabini kuhofiwa kufukiwa katika migodi ya machimbo yasiyo rasmi baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo wakati wakichimba dhahabu katika eneo la Nyakagwe, kitongoji cha Mtukula kijiji cha Kaseme, wilaya ya Geita mkoani Mwanza.
Picture
William Ngeleja/Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na Wachimbaji
Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 7 usiku wakati watu hao wakichimba dhahabu kwenye shimo lenye urefu wa futi 5 ambapo gafla waliangukiwa na kifusi cha udongo na kufa papo hapo.

Waliodaiwa kufa ni Kulwa Daud mkazi wa Mtukula, Majaliwa mkazi wa Nyarugusu, Peter mkazi wa Kaseme na Baraka mkazi wa Msasa, Geita na miili yao imeopolewa kutoka ndani ya shimo hilo.

Kamanda wa mkoa wa Mwanza Bwana Simon Sirro alithibitisha kutokea kwa uvumi huo na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Jeshi la Polisi walizuru eneo hilo.

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Geita ikiongozwa na Mkuu wa wilaya Bwana Filimon Shelutete ilisimasha shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo.

Inadaiwa eneo hilo lipo chini ya kampuni ya STAMICO na watu wamekuwa wakifanya uchimbaji kwa kujiiba.

Hata na hivyo, hakuna hata mwili mmoja uliopatikana baada ya ufukuzi wa eneo lililosadikiwa kufukia watu.

credit: habari - Na Salum Maige, Geita/RFA na picha - Mroki Mroki

Photos of Wladimir Sidorenko vs Mbwana Matumla

30/8/2010

 
Former WBA bantamweight champion Wladimir Sidorenko (22-2-2, 7 KOs) had an unanimous decision win over Mbwana Matumla of Tanzania (19-5, 11 KOs) on Saturday at the Independence Square in Kiev, Ukraine.

The three judges scored 120-108; 119-109 and 120-108.

Sidorenko now takes the vacant WBC International Silver super flyweight title.

Below are some action photos from the ring (click to enlarge a bit, sorry for the size & watermarks, that's all I got).
Picture
Mbwana Matumla (L) vs Wladimir Sidorenko (R)

Mkanganyiko wa maagizo ya Raisi wakati wa kampeni

30/8/2010

 
Raisi amwagiza wakala kuongeza ununuzi nafaka Tunduma

Raisi Jakaya Kikwete ameagiza Wakala wa Hifadhi ya Chakula (SGR) kuongeza kiwango cha ununuzi wa nafaka kutoka tani 150,000 hadi 400,000 ili kuwapa soko la uhakika wakulima.

Alitoa maagizo hayo jana kwenye mikutano tofauti ya kampeni maeneo ya Matei mkoani Rukwa na Tunduma mkoani Mbeya anakoendelea na kampeni za uchaguzi mkuu.

Rais Kikwete alirudia agizo lake la kutaka wakala huyo kununua mizani na kuongeza fedha za ununuzi wa nafaka ili kuwapa soko la uhakika wakulima ili waondokane na hatari ya kuangukia kwenye mikono ya walanguzi.  "Wakala wa hifadhi ya chakula ataongeza fedha za ununuzi wa nafaka. Ukosefu wa mizani ni tatizo la kitoto... mizani inunuliwe ili kuongeza kasi ya ununuzi," alisisitiza.

Mbali ya hatua hiyo, Rais Kikwete alisema serikali itajenga bandari ya Kasanga mkoani Rukwa na kuimarisha barabara ili kurahisisha huduma ya usafiri katika ya eneo hilo na Zambia, hivyo kuwaondolea wananchi adha wanazopata kwa sasa.

Kwa upande wa wananchi wa Tunduma, Rais Kikwete alisema Serikali itajenga hospitali ili kupunguza adha wanazopata wananchi katika kupata huduma za afya, ambapo kwa sasa wamekuwa wakitegemea kituo cha afya. Aliongeza katika kutatua kero ya magari ya mizigo kulundikana upande wa Tanzania katika mpaka wake na Zambia, alisema kiongozi wa nchi hiyo (Rais Rupia Banda wa Zambia) amekubalia kusaidia kutatua kero hiyo. Alisema Serikali itahakikisha kero ya maji na umeme inatatuliwa katika kipindi kifupi kijacho na kuwaomba wananchi kumpigia kura yeye na wagombea wengine wa CCM ili aweze kutimiza ahadi alizotoa.

Awali, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Profesa Mark Mwandosya, akimkaribisha Rais Kikwete alisema eneo la Tunduma lina tatizo la maji la muda mrefu ambalo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi, licha ya jitihada za Serikali za kutoa sh. milioni 500 kutatua kero hiyo.

credit: Bakari Mnkondo, Tunduma/Uhuru

YATOKANAYO

Ninagusia suala moja tu, 'agizo' la Raisi kwa Wakala. Nawaza na kujiuliza ikiwa agizo hili la Raisi latolewa kama Raisi katika shughuli zake za Kiserikali au kama Mgombea wa Uraisi kupitia CCM katika kampeni?

Sina ufahamu wa miiko ya Katiba na Sheria ya Uchaguzi, hivyo mniwie radhi kwa kuwaza hivi, pengine ikipelekwa kesi mahakamani au ukapotolewa ufafanuzi, nitapata uelewa wa kunisaidia kutofautisha kauli za Raisi wa nchi kwa sasa dhidi ya kauli za Mgombea wa Uraisi kupitia CCM ambaye ni Raisi wa nchi kwa sasa.

Nasema hivi kufuatia kauli ya CHADEMA kuishitaki CCM/Raisi Kikwete kwa anaosema na kuagiza ndani ya kipindi hiki cha kampeni, inakuwa kama "unfair advantage"  kwa kuwa yeye ni Raisi kisha anagombea Uraisi.

Yaani ni sawa na kusema kwamba, kwa vile yeye kwa sasa ni Raisi na vile vile yeye ni mgombea Uraisi, basi anatumia kofia mbili kama msumeno kukata kuwili, yaani kutoa agizo kama Raisi na kisha kufanya kampeni kama Raisi mtarajiwa. Unakosekana mpaka (a clear demarcation) wa hili ni agizo haliingiliani na sera. Je, ilipaswa auze sera za CCM Tunduma kisha aondoke, na apange safari nyingine upya, au akiwa katika ofisi yake ya Kitawala, atoe agizo kama Raisi kuhusu Wakala wa ununuzi Tunduma? (waweza kubadili pia kuwa alipaswa atoe agizo kama Raisi na kisha afunge safari ya kampeni ambayo hapaswi kutoa maagizo bali kunadi sera zake).  Kwa ilivyo sasa, ni vigumu sana kutofautisha (1) Aliyefika hapa na kutoa agizo ni Raisi wa nchi Jakaya Kikwete na (2) Aliyefika hapa ni Mgombea wa Uraisi Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete.

Sijui nimejieleza sawa au ndo nimezidi kujichanganya kisha nikalikogora? arrrggggh! eniwei, ndo hivyo hivyo.

Huku juu ndo' pa kudakia sera 'fasta' zikiwa za moto

30/8/2010

 
Picture
Wakiwa juu ya mti kama ndege katika viota ni wananchi waliokuwa wakifuatilia mkutano wa kampeni za CCM Iringa.
Siyo Wakerekewa wa CHADEMA tu ati wajua kukwea miti kuketi kiotani, a-a, ipo hata kwa waCCM hiyo.

Ujue Baba zetu ni hao haoo, Mama zetu ni wale walee, na Watoto wao ni sisi sisii, sema tu tafauti zetu ni itikadi. Tabia je? ni zile zilee...? mmh!

Nyumba inapangishwa Kijitonyama

30/8/2010

 
Nyumba inapangishwa iko maeneo ya Kijitonyama ina vyumba viwili kimoja ni self contained. Ina sebule, jiko car parking na choo cha nje. Bei ni Sh. 250,000/- Kama unahitaji wasiliana na Amani 0715154070
<<Previous
    Picture
    Get professional advise for a Tanzanian or UK visa. Contact T UK Visa consultancy, C: +255 222 139 502 or E: info@tukvisaconsultancy.co.tz

    Archives

    February 2014
    January 2014
    December 2013
    November 2013
    October 2013
    September 2013
    August 2013
    July 2013
    June 2013
    May 2013
    April 2013
    March 2013
    February 2013
    January 2013
    December 2012
    November 2012
    October 2012
    September 2012
    August 2012
    July 2012
    June 2012
    May 2012
    April 2012
    March 2012
    February 2012
    January 2012
    December 2011
    November 2011
    October 2011
    September 2011
    August 2011
    July 2011
    June 2011
    May 2011
    April 2011
    March 2011
    February 2011
    January 2011
    December 2010
    November 2010
    October 2010
    September 2010
    August 2010
    July 2010
    June 2010
    May 2010
    April 2010
    March 2010
    February 2010
    January 2010
    December 2009
    November 2009
    October 2009

    RSS Feed

    .
Powered by Create your own unique website with customizable templates.